Tangazo Muhimu:

Karibu katika tovuti ya IFM Fellowship CCR,Tafadhali jiskie huru kutoa maoni yako juu ya hii tovuti.

Tuesday, June 21, 2016

UNA NINI CHA KUTUFUNZA KUHUSU SILVER JUBILEE YA DR ALEX LENGEJU? Soma ushuhuda mzito wa Annamaria Nzamba hapa!!!

Jana nilikuwa na wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi kuhusu kuhudhuria jubilee ya Mr and Mrs Alex Victor Lengeju ama la... Ishu ilikuwa ndani yangu nasikia sana kwenda kuwapasupport kutokana na namna ambavyo waliwahi kujitoa sana kwetu, yaani sana na sio kwamba tuliwaomba, hapana ni wao tu walijitoa. Lakini sasa naendaje wakati sina hata mtu wa kubaki na hawa watoto.... Ndani yangu nilikuwa napambana nini nifanye... Mpaka mwisho nikaamua niende itakavyo kuwa ndio hivyo hivyo.... My children won't die kwa changamoto ya siku moja...
Unajua ningeamua kubaki hakuna ambae hasingenielewa katika hali ile, ila msukumo wa kwenda ulikuwa mwingi tena mkubwa, miaka 25 ya ndoa? Nani hasiyetamani upako Kama huo...? So nikabeba wanangu, nikaenda..
Labda nifupishe tu kwa kusema kwamba, mpaka nimeamua kuandika hapa, kipo cha ziada nilikutana nacho..
Ule wasi wasi wa kuhusu itakuwaje, Mungu aliniletea wasaidizi toka mbinguni wenye upendo wa ajabu sana yaani mlinibariki wapendwa jamani mweh... Alianza dada Jacque Siara akamchukua Archangel, mara kaka Epimack Mbeteni akambeba Annointing mara Chrispin Chalyaakasaidia kukaa na Annointing rafiki yake, Leah Kibode mpenda watoto akampokea mara Sway Gabriel Perfect akamchukua Archangel akacheza nae kwaito, bila hata kukataliwa... Sijakaa sana da Tumaini Mfujege naye akamchukua Annointing mara tena kaka Epimack tena Leah, Perfect akajaribu kumchukua Aki this time akakataliwa, sijui ulimfinya mwanangu?
Kaka Michael na Aneth Meela mke wako mlikuja mkanitia moyo...
Haikutosha, wakati wa kwenda kuchukua chakula nikiwa na watoto kwenye foleni nikashtukia Regina huyu hapa, kawaomba radhi waliokuwa kwenye mstari , "samahanini sijawaruka, nataka kumsaidia watoto huyu dada" mweh jamani Regina!!! Na hali yako wala hukujali jamani... Mmh hadi natokwa machozi, Avit Temu nifikishie salamu. Mwanangu akapakuliwa akabebewa chakula mpaka kwenye kiti , tunaanza kula bado wakatokea watu wakaniwahi usimpe chakula mtoto kina pilipili Sana. Nakumbuka Tumaini ulikuja toka mezani kwako mpaka kwetu ukaulizia mtoto Kala nini ili tu kumlinda na ile pilipili....
Huu upendo wenu sina namna ya kuulipa ... Nimeguswa sana sio kichekesho nimeamua kuandika, na wala sio kwamba sina cha kufanya, kuna kitu kikubwa Mungu ananifundisha kupitia kwetu, Namsihi Mungu anikumbushe kupenda wengine, na kujitoa sadaka kwa wengine kama mlivyojitoa kwangu....
Sijui mliona nini labda au sijui mlisukumwa na nini labda, what ever the reason or no reason.... I pray to God that He will shower his abundant blessing upon you maishani mwenu... Mungu awabarikini na anipe kuukumbuka upendo huu.
Sijawasahau na wengine wengi kule fellowship ambao hamchaacha kuwa msaada.... Nawakumbuka wote... Kuna waliomkuta Anno anaumwa wakamuwekea mikono wakamuombea, I bless you all.
Hakika through this fellowship ninaonja kuishi kwa kumegeana mkate kama mitume...
Hamjaacha kunibariki. Asanteni nyote kwa upendo wenu.
Share

Ifm Fellowship

IFM Fellowship is a Christian youth based fellowship that brings together more than 60 youth to learn, praise,worship and glorify Jesus Christ in their life.

0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2013 IFM CCR. Template by: Templateism