HUDUMA YA KUSIFU NA KUABUDU (PRAISE & WORSHIP)
Lengo kuu hasa ni kushiriki katika kuujenga mwili wa Kristo. Huduma hii imeanza tangu kikundi hiki kimeanzishwa na kinakua siku hadi siku kwa jinsi Mungu anavyozidi kutuinua.
Kusifu na kuabudu ni ibada ya kutangaza/kukiri sifa, ukuu, uweza, mamlaka, enzi uumbaji, na utukufu wa Mungu wetu anayeishi. Mungu anatafuta moyo unaomwabudu katika kweli. Na yeye ni Mungu anayekaa katika sifa
Pia huduma hii inatulea ili tuishi maisha ya uchaji na kuunganisha kile tunachotangaza kuhusu Mungu na maisha yetu.
Wanahuduma tunakutana kwa wiki mara mbili jumatano maombi na jumamosi ni mazoezi, pia tunakuwa na mafungo ya siku nzima kila baada ya miezi mitatu ili kuutafuta uso wa Mungu.
Mwanachama anayetaka kujiunga lazima uwe unampenda Mungu, unapenda kuimba sifa zake na tayari kujitoa sadaka kwa muda wako kwa ajili ya Mungu, maana ni huduma ambayo inahitaji sana sadaka ya muda kwa ajili ya mazoezi.
Pia kuna kanuni zetu kwa mfano kila mwanachama mpya atakaa ndani ya huduma kwa muda wa miezi mitatu ndipo tunamruhusu kuhudumu. Lazima awe ameshapitia semina za maisha ya kiroho au asome semina za maisha ya kiroho kama hajasoma, awe mtii na mnyenyekevu sio kwa viongozi tu bali kila mtu. Hizo ni baadhi.
Huduma hii tunatarajia kuzindua rasmi jina la kwaya yetu mwezi wa kumi na moja mwaka huu 2013, na baada ya hapo mwaka kesho tunakusudia kuhifadhi (record) nyimbo zetu mpya tulizotunga wenyewe.
Pia kwaya hii inajumuika na kwaya ya umoja wa vyuu vikuu kwenye zile huduma za pamoja kama Usiku wa sifa na compus crusade.
Pia huduma hii tuna mlezi ambaye anatushauri na kutulea katika kusudi la Mungu na anakuwa karibu na sisi kutufundisha na kutuelekeza namna ya kumtumikia Mungu ktk uimbaji. Pia tuna mwalimu tunayeshirikiana naye katika huduma na mazoezi