Tangazo Muhimu:

Karibu katika tovuti ya IFM Fellowship CCR,Tafadhali jiskie huru kutoa maoni yako juu ya hii tovuti.

Historia

HISTORIA YA IFM FELLOWSHIP,CCR.

Kikundi cha sala cha IFM, kilianzishwa tarehe 25/03/2007 chini ya uongozi wa karismatik katoliki jimbo kuu la Dar es salaam.
Madhumuni ya uanzishwaji ni kuamsha imani za wakatoliki na kanisa kwa ujumla ndani ya chuo cha IFM,vyuo vingine pamoja na parokia ya St Joseph.

Kikundi hiki tangu kimeanzishwa mpaka sasa kinakutana kwa ibada parokiani St. Joseph kila jumapili kuanzia saa 10 jioni.

Kikundi kilianza na takribani idadi ya watu kumi (10) na imekuwa ikiongezeka siku kwa siku na sasa tupo takriban ya watu mia moja.

Wakati wa mikutano ya sala huwa tunafanya mambo yafuatayo;

1. Kufungua kipindi kwa sala
2. Kusifu na kuabudu
3. Neno la Mungu
4. Maombi
5. Matangazo na kushirikishana amani.

Copyright @ 2013 IFM CCR. Template by: Templateism