Kikundi cha sala cha IFM, kilianzishwa tarehe 25/03/2007 chini ya uongozi wa karismatik katoliki jimbo kuu la Dar es salaam.
Madhumuni ya uanzishwaji ni kuamsha imani za wakatoliki na kanisa kwa ujumla ndani ya chuo cha IFM,vyuo vingine pamoja na parokia ya St Joseph.
Kikundi hiki tangu kimeanzishwa mpaka sasa kinakutana kwa ibada parokiani St. Joseph kila jumapili kuanzia saa tisa na nusu hadi saa kumi na moja na nusu (15:30-17:30) jioni.
Lakini pia kwa kila jumapili ya kwanza ya mwezi huwa tunakutana kwa masaa takriban matatu katika ukumbi mojawapo katikati ya jiji ambapo kwa sasa tumekuwa tukitumia sana HIDERY PLAZA POSTA MPYA.
Kikundi kilianza na takribani idadi ya watu kumi (10) na imekuwa ikiongezeka kwa kasi siku kwa siku.
karibuni sana tena jumapili hii kwa ajili ya kuendelea na kumsifu , kumwinua MUNGU na kuendelea kujifunza neno lake.
ni pale kanisa la MT YOSEFU katika ukumbi wa wawata ulipo nyuma ya kanisa mara uingiapo kupitia geti kuu.
kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo:
0717 203 772, 0752 507 171, 0656 516 903, 0658 123 232
IFM Fellowship is a Christian youth based fellowship that brings together more than 60 youth to learn, praise,worship and glorify Jesus Christ in their life.
0 comments:
Post a Comment