Tangazo Muhimu:

Karibu katika tovuti ya IFM Fellowship CCR,Tafadhali jiskie huru kutoa maoni yako juu ya hii tovuti.

Tuesday, June 21, 2016

HATA UKIWA KWA YESU LAZIMA KUPENDEZA BWANA!!

 Vunja kabati kwa ajili ya Bwana!!!
Na Anamaria Nzamba
Da Tumaini Mfujege somo lako la jumapili iliyopita niliguswa na ule ushuhuda wako hasa pale uliposema, "...baada ya kufunga na kuomba, siku ya kufungua, hali ukijua na ukiamini ulikuwa umefufuka, uliamua kuvaa kifufuko fufuko...." uuuuuuuuuh of coz yes, tena ukatupia kitu cha silver, nguo yako ya kusimamia maids, ukatoka kifufuko... I loved this. ndio maana nimeamua kuandika hapa.
Bwana Yesu nakuhitaji niwezeshe kuandika kwa namna ambayo itakupendeza wewe Zaidi na watu wako kwa ajili ya sifa na utukufu wa jina Lako. Unihurumie eeh Yesu wangu. Ninapenda kukutumikia kwa moyo wangu wote, kwa nguvu zangu zote na kwa uwezo na akili zangu zote. Amen
Kuvaa kifufuko: ukweli kabisa mimi ninaamini katika hili, kama mkristu niliyekombolewa sina budi kuwa na muonekano ambao utanitambulisha katika jamii, kwamba nimefufuliwa, nimekombolewa, Yesu yuko ndani yangu, nami ndani yake, Yesu ananipenda, nami nampenda, ninalindwa, ninamsaada ooh niko na Yesu... etc etc
nikikumbuka hayo yooote, siwezi kuacha kuvunja kabati kila siku iitwayo leo, aliyefufuliwa na Yesu hata kimuonekano tu utamgundua. Anavaa vizuri, anapendeza, na kupendeza haihusiani na gharama kabisa, kuna nguo za kila aina na bei rahisi nzuri ajabu... tupendeze jamani. hebu tuwe tunavunja kabati, maana ukweli kabisa kila siku ni siku mpya na Bwana amejifunua kwetu karibia kila siku. kila mtu anao ushuhuda wa kila siku, sasa kwa nini kama tunafufuliwa kila siku , hatupendezi kila siku...!

Tuko radhi kupendeza kazini lakini sio kanisani. Tuko radhi kupendeza kwenye harusi lakini sio fellowship, take this as a challenge, pendeza mtu wa MUNGU! narudia tena pendeza! unajua muonekano wako ni mahubiri tosha... ukivaa unahubiri na hayo mavazi yako... vaa kifufuko watu waone kwamba kwako wewe kuna uhai kila siku, kuna ufufuko kila siku....
Kusema kweli kuna wakaka na wadada wa fellowship nawaadmire sana mko juu, mnadhihirisha kuwa mmefufuliwa in and out... safi sana. Mnajitahidi sana, sio gharama bali kupendeza.
na ukijua kuvaa kifufuko, utajua kula kifufuko, kuishi katika nyumba za kifufuko, yaani watu wakija kwako hutokuwa na sababu za kuwaficha jikoni, au kutowakaribisha ndani... kwako kuking'ara hata wewe utang'ara. narudia tena, siongelei kuwa na vitu vya gharama, naongelea kuwa na vitu vizuri, vinavyopendeza.
Mtu ni mwili na roho, hata sisi YESU ametukomboa mwili na roho, ushishughulikie tu ya rohoni, ukasahahu ya mwilini, chukua hatua, fanya kitu kwa ajili ya mambo ya mwilini pia, kuanzia mwili wako na mazingira yako yambariki MUNGU na sisi wengine.
Mi ninaamini kabisa katika kupendeza kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja na ukiroho wa mtu husika. Tena kanisani kuwe Zaidi hata ya ofisini, fellowship kuwe Zaidi hata ya kwenda kwenye interview....
Tuma, nilikuelewa sana. Mimi Bwana ananifufua kila siku, nitahakikisha natokelezea kifufuko fufuko kila siku.
Wapendwa mbarikiwe sana.
Share

Ifm Fellowship

IFM Fellowship is a Christian youth based fellowship that brings together more than 60 youth to learn, praise,worship and glorify Jesus Christ in their life.

0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2013 IFM CCR. Template by: Templateism