Kutoka kwenye somo la jumapili hii iliyopita aliyofundisha bro. Lordswill Paul niliguswa Sana. Conflict within a man. Unatamani kufanya hiki lakini kuna kitu kingine kinakuzuia na ndani yako unapambana... Akasema kuna watu hapa wangejua kama maisha yako hivi, yako mambo ambayo yalifanyika huko nyuma, wasingeyafanya kabisa....!
Haleluya! Tumsifu Yesu Kristu!
Ni kutokana na maneno hayo mimi nimesikia mzigo sana kushare haya machache... Namsihi Mungu aachilie pumzi Yake katika neno hili ili likawe hai kwa mtu fulani. Ili likabadilishe maisha ya mtu fulani.
Ni kutokana na maneno hayo mimi nimesikia mzigo sana kushare haya machache... Namsihi Mungu aachilie pumzi Yake katika neno hili ili likawe hai kwa mtu fulani. Ili likabadilishe maisha ya mtu fulani.
Naongelea uaminifu. Wapendwa kutokuwa muaminifu kunachafua sana hali ya mtu. Usipokuwa muaminifu ni rahisi kutenda dhambi. Na dhambi ni mbaya kuliko unavyoweza kujua. Ni mbaya mno. Dhambi inakuchafua
Dhambi ina inakurudisha nyuma
Dhambi ina leta mapooza kiroho
Dhambi inakuondolea kibali
Dhambi inakukosesha baraka
Dhambi inakutenga na Mungu
Dhambi inaleta umauti
Dhambi ni kifo!
Dhambi ina inakurudisha nyuma
Dhambi ina leta mapooza kiroho
Dhambi inakuondolea kibali
Dhambi inakukosesha baraka
Dhambi inakutenga na Mungu
Dhambi inaleta umauti
Dhambi ni kifo!
Ndugu yangu unafanya nini unapokuwa sirini? U muaminifu? Kama Mungu akiamua kuweka TV na kuonesha maisha yako yooote walau kwa mwezi huu tu, tangu unapoamka hadi unapoenda kulala kwa siku zote mwezi huu, utakuwa na ujasiri wa kiruhusu hilo?
Ningeweza kukuonesha athari za kukosa kwako uaminifu ningeshika akili yako na fikra na kila kitu mpaka uelewe. Maana athari zake ni kubwa mno ni nyingi mno. Unajua utakuwa wapi baada ya miaka mitano kwa mfano? Unajua mbele yako iko changamoto gani mpendwa? Sasa kwa nini usiweke hazina ya uaminifu sasa ili ije ikufae wakati wa dhiki yako? You need to be serious my dear. Ufalme wa Mungu unatawaliwa na wenye nguvu, walio serious na maisha, sio wazushi wazushi, sio waongo au wezi au wenye Mizaha sio wanafiki wala wazinzi sio wambea wala wapenda rushwa BALI wenye nguvu katika kulitafari neno la Mungu na kuliishi bila woga bila unafiki.
Itafika wakati utakutana na changamoto kubwa katika ndugu zako, labda unakuta kuna ugomvi mkubwa kwa ndugu wa ukoo ambao unakuathiri hata wewe, saa ngapi utaweza kupigania ushindi ndugu yangu na hali wewe hukujali wokovu wako?
Labda watoto wako watakuja kukamatwa na kitu cha ajabu sana huko mbele na wewe pamoja Na miaka yote hiyo ya kumtumikia Mungu huna nguvu hata kidogo kuweza kuwasaidia wanao na hapo labda unaishi vijijini huko. Kisa, wakati wa kukua kiroho wewe ulipuuza hukuzingatia ukakosa uaminifu....
Sikia Nikwambie, kuna malengo yako unayoyatamani hapo mbeleni labda kuwa muimbaji mkubwa, kuwa kiongozi wa taifa au kuwa na familia bora au vyovyote upendavyo.... Nakusihi Sana zingatia uaminifu ili uweze kuyafikia hayo malengo yako, acha dhambi, maisha sio rahisi kiasi hiko.... Jitahidi Sana, sio tu wewe kumuamini Mungu, hakikisha na yeye Mungu anakuamini.
Yahitajika uaminifu. Kazini wahi, chapa kazi. Tumika. Nyumbani pia, kwenye familia yako kuwa muaminifu Hata kama hakuna anayekuona, darasani acha kudesa. Fellowship wahi, fika usitege. Hudhuria pia kwenye huduma acha excuses wahi, uparticipate fully. Fungu lakumi pia toa. Yaani timiza wajibu wako kila mahali shetani asipate cha kukuhukumu akaiba taji na ushindi wako...

Panda mbegu nzuri sasa uje uvune nazo mazuri baadae. Huu ni wakati wa kujiongezea nguvu katika Bwana, huu ni wakati wa kukua kiroho , huu ni wakati wa kupambana kuifikia taji yako. Usipitwe na kasi hii. Kuwa muaminifu na utamuona Bwana.
Ni kweli Mungu anasamehe, lakini hata akikusamehe kuna mahali hutofika! Muulize mfalme Daudi ambaye alifanyika najisi kwa dhambi aliyoitenda... Hakuweza tena kumjengea Mungu hekalu... Na Ukizingatia Daudi is termed as a man after God's heart..... sembuse mimi na wewe...? Tuache dhambi! Tuwe waaminifu ili tusije kujuta baadae.
Ninajua ninachokiongea. Ninajua. Ndio maana ninawiwa juu yako.
Ooh neno hili na lipate kibali kwako.
Amen
Ninajua ninachokiongea. Ninajua. Ndio maana ninawiwa juu yako.
Ooh neno hili na lipate kibali kwako.
Amen
IFM Fellowship is a Christian youth based fellowship that brings together more than 60 youth to learn, praise,worship and glorify Jesus Christ in their life.
0 comments:
Post a Comment