Vunja kabati kwa ajili ya Bwana!!!
Na Anamaria Nzamba
Da Tumaini Mfujege somo lako la jumapili iliyopita niliguswa na ule ushuhuda wako hasa pale uliposema, "...baada ya kufunga na kuomba, siku ya kufungua, hali ukijua na ukiamini ulikuwa umefufuka, uliamua kuvaa kifufuko fufuko...." uuuuuuuuuh of coz yes, tena ukatupia kitu cha silver, nguo yako ya kusimamia maids, ukatoka kifufuko... I loved this. ndio maana nimeamua kuandika hapa.
Bwana Yesu nakuhitaji niwezeshe kuandika kwa namna ambayo itakupendeza wewe Zaidi na watu wako kwa ajili ya sifa na utukufu wa jina Lako. Unihurumie eeh Yesu wangu. Ninapenda kukutumikia kwa moyo wangu wote, kwa nguvu zangu zote na kwa uwezo na akili zangu zote. Amen
Kuvaa kifufuko: ukweli kabisa mimi ninaamini katika hili, kama mkristu niliyekombolewa sina budi kuwa na muonekano ambao utanitambulisha katika jamii, kwamba nimefufuliwa, nimekombolewa, Yesu yuko ndani yangu, nami ndani yake, Yesu ananipenda, nami nampenda, ninalindwa, ninamsaada ooh niko na Yesu... etc etc
nikikumbuka hayo yooote, siwezi kuacha kuvunja kabati kila siku iitwayo leo, aliyefufuliwa na Yesu hata kimuonekano tu utamgundua. Anavaa vizuri, anapendeza, na kupendeza haihusiani na gharama kabisa, kuna nguo za kila aina na bei rahisi nzuri ajabu... tupendeze jamani. hebu tuwe tunavunja kabati, maana ukweli kabisa kila siku ni siku mpya na Bwana amejifunua kwetu karibia kila siku. kila mtu anao ushuhuda wa kila siku, sasa kwa nini kama tunafufuliwa kila siku , hatupendezi kila siku...!